Tuesday, October 2, 2012



ADVERTISEMENT

MONDAY, OCTOBER 1, 2012

JOSE MOURINHO: NINAYACHUKIA MAISHA YANGU

Unaweza ukadhani mwanaume anayeamini kwamba yeye pekee ndio anastahili kuitwa "The Only One" angeweza kupenda namna anavyopata mapokezi ya aina yake huko mitaani anapoenda kutembea, lakini kwa Jose Mourinho ungeweza ukawa umekosea. Kocha huyo wa Real Madrid anasema hana furaha na maisha yake ya kawaida anayoishi mitaani.

Kutoka the Independent:

"Kama ningeweza kuwa kocha, kocha wa soka, kwa muda huu nikaondoka klabuni baada ya mechi na kuzima mwanga wote na kuwa mtu mpya ambaye hakuna mtu anayemjua, nigefanya kazi hiyo vizuri kwa raha," aliambia CNN.

"Kwasababu nayachukia maisha yangu ya kawaida. Sipendi maisha ya ustaa. Nachukizwa sana na kushindwa kuishi maisha ya kawaida, kama baba ambaye anaenda na mwanae wa kiume kuangalia soka na kuwa pale na wababa wengine 20 tunaangalia mchezo huo.

"Nipo kwenye mechi ya soka ya watoto wa miaka 10-12 na ninatakiwa kuwepo pale, watu 
wanakuja na kuanza kuomba kupiga nao picha, washabiki wanakuja kwa kutaka kupata saini,Wengine wanakuja kunitukana tu, wengine huenda golini kwenye lango analodaka mwanangu mwenye miaka 12 na kumtukana mwanangu."


CHAMPIONS LEAGUE: VAN PERSIE NA ROONEY KUJIULIZA KWA WAROMANIA - BENFICA NGOMA NZITO DHIDI YA BARCELONA

RATIBA YA MECHI ZA LEO ZA LIGI YA MABINGWA WA ULAYA

Kundi E
    Juventus         v Shakhtar Donetsk       (saa 3:45) usiku
    Nordsjaelland    v Chelsea                    (saa 3:45) usiku

Kundi F
 
    Valencia      v Lille                                 (saa 3:45) usiku
    BATE Borisov  v  Bayern Munich         (saa 3:45) usiku
    
Kundi G

    Benfica        v Barcelona                       (saa 3:45) usiku
    Spartak Moscow v Celtic                       (saa 1:00) usiku
   
Kundi H
 
    CFR Cluj       v Manchester United        (saa 3:45) usiku
    Galatasaray    v Braga                            (saa 3:45) usiku

GOLI LA SIKU: FABRIZO MICCOLI AFUNGA BAO TAMU KIBOKO YA YOTE SERIA A

UDANGANYIFU HUU WA WACHEZAJI WA BARCELONA UNAHARIBU SIFA YAO


Cesc Fabregas aliisadia Barcelona kupata ushindi dhidi ya Sevilla katika njia zaidi ya moja, akiisadia Barca kushinda mechi ya sita mfululizo kwenye La Liga.

Huku Barca wakiwa nyuma kwa 2-0, Fabregas akafunga bao dakika ya 53lilowasaidia watoto wa Vilanova kurudi mchezoni, lakini pale alimpodanganya refa na kusababisha kiungo wa Sevilla kutolewa nje kwa kadi nyekundu ndipo alipoisadia timu kubadilisha matokeo kuwa mazuri upande wao.

Fabregas alimdanganya refa kwamba mchezaji wa Sevilla amempiga kichwa na hivyo kupelekea Sevilla kucheza pungufu na Barca wakatoka nyuma na kufunga mabao mawili yaliyowapa ushindi dhidi ya Sevilla na kuendelea kuongoza ligi hiyo.

Vitendo vya udanganyifu kwa wachezaji wa Barcelona vimekuwa vikichafua sifa nzuri ya klabu hiyo ya kucheza kandanda safi na lenye mvuto.

WACHEZAJI WA YANGA WALIVYOWAFANYA POLISI KUSAHAU KAZI YAO UWANJANI


WASHIRIKI WA EBSS WALIVYOFUNGUKA KATIKA SHOW YA JANA USIKU

-->
CAESAR DANIEL MTANGAZAJI WA EBSS AKIPOZI KWA AJILI YA PICHA NA WASHIRIKI WA EBSS, VINCENT MUSHI (KUSHOTO) NA GODFREY  LEVIS (KULIA).

--> CAESAR DANIEL AKIPOZI KWA AJILI YA PICHA NA MSHIRIKI WA EBSS NORMAN SEVERINO
--> CAESAR DANIEL AKIPOZI KWA AJILI YA PICHA NA WASHIRIKI WA EBSS WABABA MTUKA(KUSHOTO) LINIAS MHAYA(KULIA)
--> MSHIRIKI WA EBSS WALTER CHILAMBO
-->
HUSNA NASSOR(KULIA) NA NSAMI NKWAMBI (KUSHOTO) WAKIPOSE KWA AJILI YA PICHA

-->
WATANGAZAJI WA EBSS CAESAR DANIEL AND VANESSA MDEE

-->
MENYNAH ATIKI AKIWA JUU YA JUKWAA

--> : NSHOMA NG’HANGASAMALA AKIPERFORM JUU YA JUKWAA
-->
: SALMA MAHIN JUU YA JUKWAA

-->
: SALMA YUSUF AKIINGIA JUKWAANI

KWANINI NISIAMINI BAADHI YA VIONGOZI WA VILABU WAMEZISALITI TIMU ZAO KWENYE UDHAMINI WA LIGI

 
Na Somoe Ngitu, gazeti la NIPASHE

WAKATI Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ikiwa inaendelea na joto la wapenzi wa mchezo huo likiwa ni katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba utakaofanyika keshokutwa kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bado najiuliza kwamba, kimeishia wapi kile kilio cha viongozi wa klabu kuhusiana na dau la udhamini wa ligi hiyo?


Je, ni kweli kimeisha hivi hivi kama machozi ya samaki baharini?
Katika mtima wangu, najiwa na hisia mbaya, tena mbaya sana. Nazo ni kwamba, huenda kuna viongozi wa klabu wameamua kusaliti maslahi ya waliyo wengi kwa sababu wanazozijua wenyewe.


Ndiyo. Na wala sihitaji kutumia nguvu nyingi ili kukidhi matakwa ya ile dhana maarufu katika misingi ya hukumu, nayo ni ile ya kuwa na ushahidi usio na shaka (beyond reasonable doubt).
Mtiririko wa yote yanayojiri katika sakata la udhamini wa Ligi Kuu ya Bara unatengeneza mazingira ya kuamini kwamba si bure. Wapo walioamua kusaliti klabu zao. Inawezekana si wote, lakini naamini kwamba wapo. Haki ya nani vile!


Kuna usaliti fl'ani umeingia kwenye suala hili nyeti ambalo ndio msingi wa ushindani wa ligi hiyo inayotoa wawakilishi wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa na pia kuzalisha wachezaji wengi wa timu za taifa, hasa ile ya wakubwa ya Taifa Stars.


Najiuliza kwa mfano. Kwamba je; hata kama hakukuwa na kampuni au taasisi nyingine ya kibiashara ambayo ilikuwa tayari kudhamini Ligi Kuu ya Bara, ni kweli kwamba yale madai ya klabu yalipoteza umuhimu wake?


Mimi naamini madai ya klabu kuhusiana na utata wa udhamini yalikuwa ya msingi kutokana na hali halisi ya mazingira ya mchezo huo hapa nchini ambapo klabu hutumia gharama kubwa kuwatangaza wadhamini kuliko kile wanachopata kutoka kwa wadhamini hao.


Binafsi nakumgbuka vyema. Wakati mjadala kuhusiana na udhamini wa ligi na kiwango cha pesa ambacho klabu kitanufaika kutokana na 'dili' hiyo, klabu kadhaa kama za Simba, Yanga na Azam zilikuwa mstari wa mbele katika kupigania kile walichodai kuwa ni haki yao.


Hata hivyo, kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele, ndivyo viongozi wa baadhi ya klabu walivyopotea na kutosikika waziwazi wakilalamikia yale waliyokuwa wakiyasema hadharani kuhusiana na kiwango na aina ya  udhamini. Badala yake, walioonekana kuwa mstari wa mbele katika kupigania maslahi ya klabu katika udhamini ni African Lyon pekee, ambao walijitahidi na kupata mdhamini wao binafsi ambaye hata hivyo, amekataliwa kwa maeolezo kwamba ni mshindani kibiashara na mdhamini mkuu wa ligi. Sasa Lyon wanaonekana kwenda kinyume na sera za mdhamini mkuu na wametishiwa kuondolewa katika ligi kuu.


Binafsi naamini kwamba madai ya Lyon yalikuwa ya msingi kwa sababu klabu kama yao (Lyon) inayotumia zaidi ya Sh. milioni 300 kwa msimu kushiriki Ligi Kuu ya Bara inahitaji kuona kuwa inapata angalau nusu ya gharama hizo kutoka kwa mdhamini na tena kwa wakati muafaka.

Klabu hiyo ambayo mmoja wa wamiliki wake ni  Rahim Kangezi, licha ya kuonekana kuwa na ukorofi, lakini ni wazi kwamba kinachowaponza ni 'ungangari' wao katika kupigania kile wanachokiamini.


Kwa mfano, inakuwaje mdhamini wa Ligi Kuu yenye mechi 26 kwa kila klabu 14 zinazoshiriki ligi hiyo kutoa kiasi cha Sh. bilioni 1.6 kwa msimu wakati huwa kuna mechi zaidi ya 180, huku mdhamini wa sasa wa timu ya taifa (Taifa Stars) akitoa Sh. bilioni 3.5 kwa timu hiyo yenye mechi takriban 8 ndani ya mwaka mmoja, tena karibu nusu zikiwa ni za nyumbani?

 
Wakati viongozi wa Shirikisho la Soka (TFF) walipokuwa wakifanya mazungumzo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya kuidhamini Stars, walizingatia gharama za uendeshaji na mwishowe wakafanya uamuzi mgumu wa kuchana na udhamini wa awali wa  Sh. bilioni 1.2 kwa mwaka na kusaini haraka udhamini mnono wa Sh. 3.5.


Ingawa Stars inasafiri na inacheza mechi za kirafiki ndani na nje ya nchi, mdhamini wake hugharamia baadhi ya gharama kwa timu za mataifa mengine ambazo huzialika kuja hapa nchini pia, lakini tofauti ya udhamini huo na huu unaodaiwa kukubaliwa na viongozi wa klabu ni kubwa mno kulinganisha na mahitaji halisi ya uendeshaji wa timu inayoshiriki ligi kuu.


Klabu zinazunguka katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Mbeya, Arusha, Tanga, Mwanza na Bukoba mkoani Kagera kucheza mechi za ligi na baadhi yao hujikuta wakienda kwenye kanda mojawapo mara mbili kutokana na ratiba ilivyo, hivyo kujikuta wakitumia kiasi kikubwa cha fedha kugharimia usafiri na malazi ya timu wawapo ugenini.


Ni jambo lililo wazi kwamba ni mechi chache sana ambazo walau timu hupata pesa za kupunguza makali ya gharama, na hasa zile zinazohusisha klabu za Simba na Yanga.
Kwa ufupi, mapato yatokanayo na viingilio vya mechi nyingine nyingi huwa hayatoshi hata kidogo katika kusaidia maandalizi ya timu.


Katika hali kama hii, mfuatiliaji mwingine wa maendeleo ya klabu zetu anaweza kuhoji kuwa je, ni klabu ngapi kati ya 14 zilizoridhia haki ya kipekee ambayo wadhamini wakuu wameipata?
Kwa mfano, hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia, alieleza kwamba klabu zimekuwa vigeugeu kwa kubadilisha mawazo yao kila mara wanapokutana. Alisema wazi kuwa jambo hilo limewafanya wafikie hapo walipo sasa ambapo hadi ligi ikianza, walikuwa bado hawajapokea fedha wala vifaa kutoka kwa mdhamini mkuu.


Aliwahi kueleza kwamba kuna kikao kimoja waliitisha na viongozi waliohudhuriwa walikuwa ni wa klabu tatu za Simba, Ruvu Shooting na Coastal Union. Lakini baada ya kikao hicho,  viongozi wa klabu nyingine waliodai kuwa hawako jijini, alikutana nao na walichomueleza ni kwamba walishindwa kuhudhuria kwavile walipewa taarifa ndani ya muda muda mfupi.


Inawezekana ni kweli viongozi hao walikuwa mbali na jijini Dar es Salaam ambapo vikao hivyo hufanyika. Lakini vile vile inawezekana kwamba kulikuwa na 'ujanja ujanja' wa kupitisha maamuzi kwa kuhusisha viongozi wachache.


Wakati wa maboresho ya mkataba mpya klabu zilisikika wazi zikisema kwamba zinahitaji kuona msimu huu wa ligi zawadi na fedha zinazotolewa na mdhamini zilingane na hadhi ya ligi husika,  huku wakieleza kwamba wadhamini hao hao ndio waliokuwa wakidhamini mashindano ya urembo ya Miss Tanzania na kutoa zawadi za gari na fedha taslimu (ukijumlisha thamani ya gari na fedha) jumla yake inakuwa kubwa kuliko zawadi ya bingwa wa ligi ya Bara.


Inakuaje TFF inakubali udhamini wa Sh. milioni 880 kwa mashindano ya wiki mbili ambayo bingwa wake anapata Sh. milioni 40 na shirikisho hilo hilo linaona ni sahihi kukubali Sh. bilioni 1.6 kwa ligi inayochezwa kwa kipindi kisichopungua miezi nane na kuhusisha mechi zaidi ya 180?


Kwa haya yaliyojiri wakati wa mjadala kuhusu udhamini wa ligi kuu, naamini kwamba hakuna wa kuzuia hisia zangu na pengine wafuatiliaji wengi wa soka kuwa kuna viongozi wa klabu wamesaliti klabu zao na kuweka mbele maslahi yao.


Inawezekana kwamba hivi sasa ikawa ngumu kuthibitisha ukweli wa hisia hizo. Lakini ni wazi kwamba ipo siku tutasikia undani wa kile kinachotokea sasa.


Haswa! Na tuipe subira nafasi yake. Tutasikia tu kwamba viongozi "X" na "Y" walifanya hivi na vile wakati wa mchakato wa kujadili udhamini wa ligi kuu ya Bara.
----

TIKETI ZA SIMBA NA YANGA ZINAUZWA KWENYE MAENEO HAYA KUANZIA KESHO

Tiketi kwa ajili ya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa keshokutwa (Oktoba 3 mwaka huu) zitaanza kuuzwa kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 
Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.
 
Vituo vitakavyotumia kuuza tiketi hizo kuanzia saa 4 asubuhi ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa, Kituo cha Mafuta OilCom Ubungo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Dar Live Mbagala na Kituo cha Mafuta Buguruni.
 
Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000. Watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.
 
Sh. 10,000 ni kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.
 
Wakati huo huo, mwamuzi Mathew Akrama kutoka Mwanza ndiye atakayechezesha mechi hiyo. Waamuzi wasaidizi ni Samuel Mpenzu kutoka Arusha na Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam wakati mwamuzi wa mezani ni Oden Mbaga pia wa Dar es Salaam.

PICHA YA SIKU!

SUNDAY, SEPTEMBER 30, 2012

RONALDO AFUNGA HAT TRICK YA 16 TANGU AJIUNGE MADRID - LOS BLANCO S WAKIUA DEPORTIVO 5-1


Real Madrid 5-1 Deportivo footyroom.com by footyroom

NEYMAR APIGWA RED CARD KWA KUMKANYAGA KUSUDI MPINZANIA WAKE - SANTOS IKITOKA SARE LIGI YA BRAZIL

CRISTIANO RONALDO ATAKA KUWEKA REKODI YA KUWA MCHEZAJI WA KWANZA KULIPWA £400,000 KWA WIKI

Mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anataka kuwa mcheza soka wa kwanza kupokea mshahara wa £400,000 kwa wiki, kwa mujibu chanzo cha habari cha ESPN.

Kutokana na sheria za kodi za Spain  zilivyo, Ronaldo atahitaji kufikia kulipwa mshahara wa £400,000 kwa wiki ili kuweza kupata anachokitaka kuwa mchezaji anayepokea fedha nyingi za mshahara.

Huku akiwa anavivutia vilabu vingi dunaiani, wakiwemo matajiri wa Man City na PSG, mazungumzo ya juu ya hatma ya Ronaldo yapo njiani kuanza.

Ronaldo ametoa taarifa rasmi akisema kwamba 'huzuni' yake aliyosema anayo haihusiani na mambo ya fedha. Lakini chanzo cha habari kilicho karibu na Ronaldo kinasema kwamba Mreno huyo anataka mshahara wake uongezwe mara mbili, na hili litafanya aamini kwamba klabu hiyo ipo tayari kumpigania aendeleee kubaki kwenye klabu hiyo.

Nahodha huyo wa Ureno aliwahi kuwa mchezaji anayelipwa vizuri zaidi duniani wakati akihamia Mafrid mwakak 2009, akiwa analipwa £200,000 kwa wiki, lakini kwa sasa amejikuta ameteremka mpaka kushika nafasi ya kumi duniani, akipitwa na wachezaji kama Samuel Eto'o, Wayne Rooney, Neymar na Didier Drogba pamoja na wengine watano.

Kingine, Madrid kwa sasa wanamiliki asilimia 50 ya haki za picha za Ronaldo, na sasa tayari ameshampita David Beckham kuwa mchezaji ambaye jezi zake zinauzwa sana katika ulimwengu wa soka.

Ronaldo ana mkataba na Madrid unaoishia 2015.

WACHEZAJI WAHAIDIWA MILLIONI 16 KILA MMOJA IKIWA WATAWAFUNGA SPAIN

Wachezaji wa timu ya taifa ya Belarus watapokea mara tatu zaidi ya bonasi zao za kawaida ikiwa watawafunga mabingwa wa ulaya na dunia Spaini mwezi ujao katika michuano ya kugombea kucheza kombe la dunia, shirikisho la soka la nchi hiyo (BFF) limesema juzi Ijumaa.


"Kila mchezaji atapokea $10,000 ya bonasi," Makamu wa raisi wa BFF Sergei Safaryan aliwaambia waandishi wa habari. Ikiwa itatokea droo ya aina yoyote wachezaji watazawadiwa pia, Safaryan alisema.


Belarus, ambao wapo chini kabisa katika msimamo wa kundi I baada ya kupoteza mechi zao mbuili za kwanza kwa Georgia na Ufaransa, watawakaribisha Spain jijini Minsk mwezi ujao tarehe 12. 


Wahispania wameshinda mechi yao moja tu, wakiwafunga Georgio 1-0 mwezi uliopita.

Kwa kawaida wachezaji wa Belarus wanapokea kiasi cha $3,000 kwa kushinda mechiyoyote ya mashindano.

LIVE MATCH CENTRE: YANGA 3 - 1 AFRICAN LYON - FULL TIME

Mpira umemalizika, Young Africans 3 - 1 African Lyon
Canavaro dkk 16, Nizar dkk 65, 89
Benedict 64
Stephano Mwasika anaingia kuchukua nafasi ya Oscar Joshua dakika ya 89
Dakika ya 89, Nizar Khalfan anaipatia Young Africans bao la tatu Young Africans 3 - 1 African Lyon
Nizar Khalfan anaipatia Young Aficans bao la pili dakika ya 65
Young Africans 2 - 1 African Lyon
Dakika ya 64, Benedict anaipataia African Lyon bao la kwanza
Dakika ya 60, Young Africans 1 - 0 African Lyon
Cannavaro dkk 16
Dk ya 58 yanga wanafanya mabadiliko anatoka kiiza na anaingia Bahanuzi
Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 1 - 0 African Lyon
Mpira ni mapumziko Yanga 1- 0 African Lyon
Dakika ya 30, Young Africans 1-0 African Lyon
Cannavaro dkk 16
 Dakika ya 16, Nadir Haroub 'Cannavaro' anaipatia Young Africans bao la kwanza
Dakika ya 15, Young Africans 0 - 0 African Lyon
   Mpira umeanza hapa Uwanja wa Taifa, kati ya
Young Africans Vs African Lyon
 KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA
1.Ally Mustapha 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Kelvin Yondani
5.Nadir Haroub 'Cannavaro'
6.Athuman Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Yaw Berko
2.Juma Abdul
3.Stephano Mwasika
4.Omega Seme
5.Rashid Gumbo
6.Nizar Khalfan
7.Said Bahanunzi

No comments:

Post a Comment