Thursday, October 11, 2012


BEEF ILIYOTOKEA KATI YA 50 CENT NA FRENCH MONTANA

Kutoka pande za state tunakuna na wasanii wawili ambao kiukweli kila mmoja anafanya vizuri katika game la muziki nchini Marekani.Sasa kuna kitu ambacho kimetokea leo hii asubuhi nchini marekani baada ya mtu mzima French montana kufunguka kuhusiana na kazi za mtu mzima 50 cent katika game la muziki.French montana baada ya kuhojiwa leo katika kituo cha radio nchini Marekani alifunguka na kusema kwamba 50 cent ameshuka ki muziki baada ya ile beef ambayo iliyokuwa kati yake na mtu mzima Rozay.Lakini French akuishia tu hapo kwani alisema kwamba beef hii ndiyo imemfanya 50 cent kukosa mashabiki wengi na mshabiki wengine kuamia kwa mtu mzima Rozay. French aliendelea kufunguka juu ya 50 cent na kusema Miaka michache iliyopita 50 Cent alikuwa akiuuza copi Milioni 10 kwa kila Album yake lakini kwa sasa hawezi kuuza hata copi million moja. Baada ya 50 cent kusikia maneno ya French Montana ,50 aliamua kuingia twitter na kuanza kumchana live French 


Hizo ndizo Twitter zao ambazo walikuwa wakijibishana mpaka beef kutokea
 
 

No comments:

Post a Comment