Tuesday, October 23, 2012


U HEARD YA XXL NA 255 ZIKO HAPA, UNAWEZA KUZISIKILIZA..

Posted: 23rd October 2012 by MillardAyo in News
0
Soudy-Brown
Stori kubwa ya U heard ya XXL Clouds fm october 23 inamuhusu Meneja wa kundi la TMK WANAUME Said Fela kutimuliwa studio aliyokua akiitumia na kundi lake.
Chukua time yako kumsikiliza Doreen akiwa na mkusanyiko wa stori zote muhimu za town kupitia 255 ya XXL, Ben Pol azungumza kuhusu kutomtaja mpenzi wake kwenye media, Wakili kuhusu kesi ya Lord Eyes na stori nyingine.

KAMA ULIMIS KUSIKILIZA HEKA HEKA YA LEO OCT 23, ISIKILIZE HAPA

Posted: 23rd October 2012 by MillardAyo in News
1
GEA HABIB
1
.
Kwa mujibu wa Necole Bitchie ni kwamba saa 48 baada ya Mwimbaji Chris Brown kuonekana na mpenzi wake wa zamani Rihanna wakikiss kwenye Queebey launch party in West Hollywood kitu ambacho kimefanya wengi waamini kwamba wamerudiana, Chris Brown ameonekana akiwa anatoka nyumbani kwake na mpenzi wake wa zamani Karrueche ambae siku kadhaa zilizopita alitangaza kumuacha, walitoka pamoja kila mtu na gari lake.
CB alitangaza kumuacha Karrueche akidai kwamba mrembo huyo alikua akiumia kuona urafiki wa Chris Brown na Rihanna ukiendelea.
Porsche Panamera ya Karrueche aliyozawadiwa na Chris Brown mwanzoni mwa mwaka huu, hapa Karrueche akiwa kaingia kuweka mafuta baada ya kutoka kwa Chris Brown.
.
.
.
.

KAULI YA WEUSI KUHUSU KUKAMATWA KWA LORD EYES.

Posted: 23rd October 2012 by MillardAyo in News
5
.
Msemaji wa kundi la Weusi Nikki wa Pili ametoa kauli ya kwanza toka kukamatwa kwa Lord Eyez wa kundi hilo kwa tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz.
Namkariri Nikki wa Pili akisema “kwanza hiyo ni habari ya ghafla alafu ni ya kusikitisha na kushtua, ni habari ambayo imetupa shida na mpaka sasa inatupa shida sana kwa sababu watu wengi wanatupigia simu kutuuliza inakuaje”
“Ukiangalia kwenye mitandao ya facebook na twitter kote imesambaa, unajua ukijua ukweli ni kitu cha msingi sana kwa sababu sisi pia tulikua hatufahamu kilichotokea, kwa hiyo cha kwanza tulichokifanya ni kutaka kujua kilichotokea, mfano mimi niliona kwenye mitandao kwamba Lord Eyes amekamatwa kwenye eneo la tukio yupo kwenye gari lakini kufatilia nikaja kugundua haikua eneo la tukio na sio gari hilo,  uhalifu ulifanyika alhamis na alikamatwa jumamosi” – Nikki wa Pili
“Kitu cha busara tulichoamua kufanya tumeamua kufatilia kisheria ili tujue uhalisia ni upi ili tuweze kutoa tamko kwa sababu sisi wenyewe Lord Eyez hatujamuona wala hatujaongea nae, na kingine ambacho kinasikitisha ni kwamba Lord Eyez ndio ametuhumiwa kama mtu binafsi lakini ukiangalia kwenye mitandao watu wanawashambulia weusi kitu ambacho sio sahihi kabisa, mimi Joh Makini, Bonta, G Nako tumepokea hiyo habari kama mtu mwingine yeyote” – Nikki wa Pili.
.
.
Msikilize Nikki wa Pili hapo chini..

WALE MNAOPENDA MAGARI, HII NDIO LAMBORGHINI YA 2013 MAZEE

Posted: 23rd October 2012 by MillardAyo in News
2

POLISI WAMETOA IDADI YA MASHTAKA YANAYOMKABILI LORD EYES, YAKO HAPA.

Posted: 23rd October 2012 by MillardAyo in News
4
.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela amethibitisha jeshi lake kumshikilia msanii Lord Eyes ambae toka weekend iliyopita taarifa zake zimesambaa baada ya kushutumiwa kuhusika na wizi wa vifaa mbalimbali kwenye gari la mwimbaji Ommy Dimpoz.
Namkariri Charles Kenyela akisema “ni kweli Isaac Waziri Maputo mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa tarehe 20 mwezi wa kumi usiku maeneo ya Kinondoni, kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu ni kutokana na taarifa tulizozipata kupitia kwa binti mmoja aitwae Kurushinde Hillary (22) mwenye asili ya kiburushi lakini mkazi wa Mwananyamala kwa Makoma Dar es salaam, alikamatwa siku hiyo hiyo kabla ya Lord Eyes”
“Alikamatwa kuhusiana na matukio ya wizi kwenye magari yani kuna mtindo ambao umeibuka ambapo ukipaki gari yako gari nyingine ya wezi inakuja inapaki jirani na gari yako ambapo kwa muda mfupi wanafanya utundu wao wanaoujua, wanafungua gari na kuiba mali iliyoko ndani, mara baada ya huyu binti kukamatwa katika kuhojiwa mtandao wake anaoshirikiana nao alimtaja mtuhumiwa Isaac Waziri Maputo (Lord Eyes)” – Kamanda Kenyela
Kwenye sentensi nyingine Kamanda Kenyela amesema “watu wengi wamelalamika kuibiwa laptop zao, mabegi, mifuko na hata silaha kwa maana mtu anakua anajiamini anaacha kwenye gari akiamini kwamba ameshalock lakini watu hawa na mtandao wao wamekua ni hatari kiasi kwamba wameliza watu wengi”
“Watuhumiwa hawa wawili Kurushinde na Lord Eyes tunawashikilia kwa tuhuma zipatazo 30, yani matukio mbalimbali 30 pengine yanaweza yakaongezeka ambayo yameripotiwa kutokea katika maeneo mbalimbali kama vile Mlimani City, Kijitonyama, ufukwe wa bahari kama Coco beach, kwenye kumbi mbalimbali za starehe na pia  kwenye maeneo ambayo kunakua na harusi, sehemu ambazo kunakua na magari mengi watu hawa ndio huwa wanaitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, tunawashikilia kwa makosa ya wizi”
Msikilize Kamanda Kenyela akizungumza hapo chini.

KAMA HUKUMSIKILIZA MBWIGA OCT 23 ON SPORTS EXTRA, YUKO HAPA

Posted: 23rd October 2012 by MillardAyo in News
0
Dakika za Mbwiga ndani ya Sports Extra ya Clouds Fm ni dakika ambazo kwa wanaomfaham Mbwiga huwa sio za kuziacha zikupite, baada ya kupata michapo yote ya kisport Mbwiga huwa ndio anamaliza show kwa kukupa michapo lakini kwa ubinifu wake, Mzaramo huyu atatumia uwanja mpana wa uswahili wake pamoja na ucheshi kuhakikisha unaenjoy na unapata kitu pia…. msikilize hapo chini.

UMESHAIONA HII VIDEO YA HUYU SHABIKI WA YANGA?

Posted: 23rd October 2012 by MillardAyo in News
2
Huyu ni shabiki wa Yanga ambae alihojiwa na CLOUDS TV kwenye mechi ya Yanga, jamaa ana hisia na machungu sana na timu yake… hebu mcheki.

PICHA 4 ZA MOJA KATI YA MAGARI ANAYOMILIKI RAPPER DRAKE.

Posted: 23rd October 2012 by MillardAyo in News
2
Rapper Drake wa Young Money akiwa na dada yake ambae wameshea baba.
Drake kesho oct 24 anatimiza miaka 26.
.
.
0
.
Jeshi la Polisi Arusha limekanusha taarifa zilizoenea toka jana kwamba watu wanne walifariki October 21 2012 baada ya fujo kutokea kwenye Pub Lamonte Karatu ambayo ilitangaza kwamba Barnaba angeimba lakini baadae mashabiki wakagundua waliibiwa viingilio kwa sababu hakua Barnaba orijino.
Taarifa nilizozipata usiku huo kutoka kwa mwandishi wa habari wa Mlimani Tv ziliamplfy kwamba mauaji hayo yalitokana na ugomvi wa chupa na visu.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha amesema hakuna mauaji yoyote yaliyotokea usiku huona kwamba amepigiwa simu nyingi sana na waandishi wa habari wakiulizia hizo taarifa.
Mmoja kati ya watu walioshuhudia ambae pia alilipa kiingilio kumuona Barnaba amesema kweli fujo zilitokea na watu walimpiga chupa yule Barnaba feki baada ya kumgundua ni muongo na alikua hawezi kuimba nyimbo za Barnaba kwenye stage, alikua anajikanyaga kanyaga kabla ya kuokolewa na mabaunsa kwa kutolewa kwenye hiyo pub.
Shahidi huyu aitwae Ibrahim amesema ukumbi ulikua na watu wasiopungua 200 na mpaka sasa hawajarudishiwa viingilio vyao na wala mmiliki hana time nao na wala hajapatikana uizungumzia hii ishu.
Kwa mujibu wa Ibrahim, hii ni mara ya pili kwa Pub hiyo kupeleka msanii feki… wa kwanza alikua Ally Kiba ambae watu waligundua wameibiwa lakini hawakufanya chochotemillardayo.com bado inamtafuta mmiliki wa hiyo Pub ili kupata stori kamil

No comments:

Post a Comment