Thursday, October 11, 2012


Photo: SABABU ZA MSANII "LINEX'' KUTAFUTWA NA POLISI LEO.

Janeth bundala, yule model aliyeshiriki kwenye video ya AIFOLA, kwenye kipengele kilicho onyesha akipigwa kofi na linex, amechukua RB ya kumsaka msanii linex ili amlipe kwa kofi alilompiga kwenye video hio.
Janeth amesema Linex ameshalipa gharama za yeye kuonekana kwenye video ila hakujua kama anatakiwa kulipwa kwa kofi alilopigwa, pia Janeth aliendelea kusema yupo tayari kupotezea mambo ya kupelekana polisi kama Linex atamlipa pesa anayotaka mapema.

Kwa upande wa Linex, amefunguka na kusema yupo tayari kuyamaliza haya mambo mapema kesho kwa sababu leo yupo studio anarekodi na hawezi kuonana nae leo. Linex aliendelea kusema kuwa aliposikia jambo hili alishtuka sana na hakudhani ni jambo serious kwani imeshapita miezi miwili sasa na jambo hili halikutajwa.

Janeth Bundala.

Msichana ajulikanae kama Janeth Bundala, ambae ameigiza katika video ya Aifola  ya Linex, amemshtaki na kumchukulia Rb Linex kwa madai ya udhalilishaji kwa kumpiga kofi la ukweli ukweli wakati wakiigiza kwenye video hiyo.
kwa mujibu wa Linex, Janeth alikua anadai kulipwa fidia ya shilingi millioni moja katika madai hayo, lakini Linex amemlipa shilingi laki tatu na kumalizana nae maana hakutaka mambo yawe makubwa.
kama unakumbuka kofi hilo lilishaleta kelele wakati video hiyo inatoka na Linex aliomba msamaha kupitia vyombo mbali mbali vya habari na mitandao ya jamii.

story hii imenishangaza kidogo yaani ni sawa na ukacheze mashindano ya ngumi halafu umshtaki mwenzio kakupiga lo

1 comment: